Social Icons

Pages

Friday, 3 October 2014

WENGER AELEZA ALIVYOKATAA KUMREJESHA OKWI SIMBA


Kocha Arsene Wenger wa Arsenal amekubali kusema kwamba, yeye ndiye alikataa kiungo nyota wa Barcelona wakati huo, Cesc Fabregas asirejee katika kikosi chake.
Fabregas alikubali kujiunga na Arsenal akitokea Barcelona ambayo alijiunga nayo akitokea Arsenal.

Lakini Wenger akakataa na hapana, hivyo Fabregas akaamua kuangalia njia nyingine na safari hii Chelsea kukawa mahali sahihi.

Chelsea chini ya Jose Mourinho ilikubali kutoa pauni milioni 30 kumnasa na tokea amejiunga nayo amekuwa akionyesha soka la uwezo wa juu.

Mashabiki wengi wa Arsenal, wangependa kumuona Fabregas anarejea nyumbani.
Lakini kuhusu hilo, Wenger amefafanua:

“Kweli nilisema hapana, kipindi Fabregas anataka kurudi, tayari tulikuwa tumemsajili Mesut Ozil, lakini kwenye kiungo tuna Santi Cazorla na Jack Wilshere.

“Hapa utaona kiungo tuliyekuwa tunamhitaji ni mkabaji.”
 
FULU VIWANJA