MSHAMBULIAJI
wa Cameroon, Albert Ebosse amefariki dunia baada ya kupigwa na kitu
kilichorushwa kutoka jukwaani wakati wa mechi ya Ligi ya Algeria, timu
yake JS Kabylie imesema.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 24 alipigwa na kitu hicho kigumu mwishoni mwa
mchezo kati ya JS Kabylie na USM Alger mjini Tizi Ouzou.
Taarifa
katika tovuti ya Kabylie jana imesema: "Wizara ya Mambo ya Ndani na
Serikali ya Nyumbani, kupitia Waziri Tayeb Belaiz, imeagiza uchunguzi wa
wazi uanze mara moja juu ya tukio hilo lililosababisha kifo cha Albert
Ebosse.
Majanga:
Mshambuliaji wa Cameroon, Albert Ebosse amefariki dunia baada ya
kupigwa na kitu kigumu kichwani kilichorushwa kutoka jukwaani
