REAL
Madrid imebisha hodi Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia
ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Borrusia Dortmund usiku huu kwenye Uwanja
wa Santiago Bernabeu katika Robo Fainali ya kwanza ya michuano hiyo.
Gareth Bale alifunga bao la kwanza dakika ya nne akimchambua vizuri Weidenfeller baada ya kazi nzuri ya Karim Benzema.
Isco
akafunga la pili dakika ya 27 baada ya kazi nzuri ya Benzema tena na
Mreno Cristiano Ronaldo akafunga la tatu dakika ya 57 kwa pasi ya Luka
Modric.
Bao
hilo linamfanya Ronaldo aifikie rekodi ya hasimu wake, Muargentina wa
Barcelona, Lionel Messi kufunga mabao 14 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Borrussia
sasa watahitaji ushindi wa mabao 4-0 ili kufufua matumaini ya kucheza
fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya pili mfululizo- au washinde 3-0
ili mshindi aamuliwe kwa mikwaju ya penalti.
Katika mchezo mwingine, Chelsea imefungwa mabao 3-1 na wenyeji PSG Uwanja wa Parc des Princes mjini Paris.
Bao
lililoizamisha timu ya Mreno Jose Mourinho usiku huu alijifunga beki
wake, David Luiza dakika ya 62 katika harakati za kuokoa krosi ya
Ezequiel Lavezzi.
PSG
walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya nne baada ya Lavezzi kutumia
vizuri makosa ya beki John Terry na kumtungua kipa Petr Cech kabla ya
Javier Pastore kufunga la tatu dakika ya 90 na ushei.
The
Blues walisawazisha kwa penalti dakika ya 27, mfungaji Eden Hazard
akimchambua vizuri Salvatore Sirigu baada ya Thiago Silva kumchezea
faulo Oscar kwenye eneo la hatari.
Chelsea itarejea Stamford Bridge wiki ijayo ikihitaji ushindi wa 2-0 tu ili kwenda Nusu Fainali baada ya matokeo ya leo.
![]() |
| La ushindi; Beki David Luiz akimtungua kipa wake mwenyewe Petr Cech kuipatia PSG bao la ushindi |
