
Man United, ambao ndio Mabingwa Watetezi
wa Ligi Kuu England, hawana nafasi tena kuutetea Ubingwa wao Msimu huu
ambao ni wa kwanza kwa Moyes kwani wapo Nafasi ya 7 na wapo Pointi 10
nyuma ya ya zile Timu 4 Bora.
Hali hii iliwafanya baadhi ya Mashabiki
wa Man United kukodi Ndege na kuirusha juu ya Old Trafford Jumamosi
walipocheza na Aston Villa huku ikivuta Bango kubwa: “WRONG ONE, MOYES
OUT”
Macari amesema: “Ni sahihi kusema mambo
si mazuri Old Trafford hivi sasa. Lakini Moyes apewe muda hata kama
Ndege nyingi zitaruka juu ya Old Trafford!”
Akitetea kuwa Moyes anahitaji muda kama alivyopewa Sir Alex Ferguson kujenga Timu yake mwenyewe upya.
Alisema: “Ikiwa Meneja wa Arsenal
anaweza kwenda Miaka 9 bila Kombe, napenda nifikiri Meneja wa Man United
anaweza kukaa Miezi 9 bila Watu kutaka afukuzwe!”
Aliongeza: “Ikiwa Chelsea hawashindi
kitu Msimu huu, utamwonaje Mourinho? Je atakuta hali kama hii ya Moyes
katika Msimu wake wa kwanza tu? Hakika nataka kuona nini kitatokea ikiwa
Arsenal watashindwa kuchukua FA CUP Msimu huu!”