KLABU
kubwa za Ligi Kuu Ulaya zimesema zimejisafisha baada ya Barcelona
kufungiwa kufanya usajili wa wachezaji kwa kukiuka sheria za usajili kwa
kusaini wachezaji walio chini ya umri wa miaka 18.
Chelsea,
Manchester United, Manchester City na Arsenal zimesema zote
zitazingatia sheria za FIFA juu ya kusajili wachezaji wadogo katika soka
ya England.
Barcelona
imezuiwa kusajili wachezaji katika vipindi viwili vijavyo vya usajili
kwa kukiuka ibara ya 19 ya kanuni za FIFA za usajili.
FIFA
imeituhumu akademi ya Barcelona, iitwayo La Masia kwa kumsajili
Mholanzi mwenye asili ya Nigeria aliye chini ya umri wa miaka 14, Bobby
Adekanye; na Wakorea watatu walio chini ya umri wa miaka 15, Lee Seung
Woo, Paik Seung-Ho na Jang Gyeolhee, Mfaransa Theo Chendri aliye chini
ya umri wa miaka 16 na Mcameroon Patrice Sousia aliye chini ya umri wa
miaka 14.
Pigo: Wachezaji wa Barcelona, Lionel Messi na Cesc Fabregas ambao timu yao imefungiwa kusajili
MAKINDA AMBAO HAWARUHUSIWI KUCHEZA BARCELONA
Lee Seung Woo - Korea, Cadete B (U15s)
Paik Seung-Ho -Korea, Cadete A (U16s)
Jang Gyeolhee - Korea, Cadete B (U15s)
Theo Chendri - Ufaransa, Cadete A (U16s)
Patrice Sousia - Cameroon, Infantil A (U14s)
Bobby Adekanye - Uholanzi Nigerian (U14s)
Paik Seung-Ho -Korea, Cadete A (U16s)
Jang Gyeolhee - Korea, Cadete B (U15s)
Theo Chendri - Ufaransa, Cadete A (U16s)
Patrice Sousia - Cameroon, Infantil A (U14s)
Bobby Adekanye - Uholanzi Nigerian (U14s)
Barcelona
pia imepigwa faini ya francs za Uswisi 450,000 na Chama cha Soka
Hispania francs 500,000 kwa kuvunja kanuni za usajili wa mchezaji.
Mabingwa
hao wa Hispania walichunguzwa baada ya kusajili wachezaji 10 wadogo na
kuwasajili kucheza mashindano kati ya mwaka 2009 na 2013.
Uongozi
wa Barcelona wamekuwa wakifuatiliwa tangu walipolazimishwa kusema
usajili wa Neymar kutoka Santos ni Pauni Milioni 71.5million, na si
Milioni 47.3, ukijumlisha na fedha alizolipwa Neymar na famili yake.
Rais wa zamani wa Barca, Sandro Rosell, alilaumiwa kwa kuvunja kanuni za FIFA na katika sakata hilo, akalazimika kujiuzulu.
Barcelona,
washindi wa mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa katika miaka 10
iliyopita, inamilikiwa na wanachama na inatambulika kama 'Ni zaidi ya
klabu,’.
