Social Icons

Pages

Saturday, 12 April 2014

OKWI, CHUJI WAACHWA DAR, YANGA IKIPAMBANA ARUSHA KESHO



Kiungo Athumani Iddi ‘Chuji’ amebaki Dar es Salaam huku kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Emmanuel Okwi akiwa bado kwenye mgomo.


Yanga ipo Arusha kwa ajili ya mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara ambapo ushindi ni muhimu kwao ili iendelee kuwania kutetea taji lake ambalo pia linaweza kutua Azam ikiwa watashinda mechi ya kesho dhidi ya Mbeya City.
 
Mtoa taarifa kutoka klabuni hapo amesema kuwa Yondani alirejea jana asubuhi na kujiunga kwenye msafari ulioelekea Arusha, lakini akasisitiza kuwa benchi la ufundi halijamchukulia hatua yoyote.

Taarifa za ndani za Yanga zimeeleza kuwa Chuji ameachwa Dar kama ilivyo kwa Okwi ambaye anaendeleza mgomo wa kutaka malipo yake.

“Ila bado anaonekana Chuji amekuwa mtovu wa nidhamu, mara kwa mara anafanya makosa, anaomba radhi, halafu anarudia mara nyingine,” alisema.

Mgomo wa Okwi, inaelezwa anadai dola 40,000 ambazo zimebaki katika dola 100,000 alizotakiwa kulipwa.

Hakuna kiongozi wa Yanga aliyejitokeza kulizungumzia suala hilo zaidi ya wale wa benchi la ufundi ambao wamekuwa wakisisitiza kuwa ni suala kati ya Okwi na uongozi        .
www.fuluviwanja.blogspot.com
 
FULU VIWANJA