KIKOSI
cha Azam FC kinachowakosa nyota wake kadhaa kesho kitakuwa na kibarua
kigumu mbele ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani
Pwani, uwanja ambao 'maafande' hao hawajapoteza hata mechi moja tangu
kuanza kwa msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Meneja wa Azam FC, Jemadari Said alisema jana kuwa kikosi chao kitakosa huduma za Samih Nuhu, Joseph Kimwaga, Ismail Gambo, Farid Mussa na Ibrahim Mwaipopo ambao wote ni majeruhi kwa muda mrefu sasa pamoja na mchezaji wao chipukizi Bryson Raphael aliyerejea jana akichechemea kwa maumivu ya kifundo cha mguu kutoka Kenya alikokwenda kuichezea timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 (Ngorongoro Heroes).
Meneja wa Azam FC, Jemadari Said alisema jana kuwa kikosi chao kitakosa huduma za Samih Nuhu, Joseph Kimwaga, Ismail Gambo, Farid Mussa na Ibrahim Mwaipopo ambao wote ni majeruhi kwa muda mrefu sasa pamoja na mchezaji wao chipukizi Bryson Raphael aliyerejea jana akichechemea kwa maumivu ya kifundo cha mguu kutoka Kenya alikokwenda kuichezea timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 (Ngorongoro Heroes).
TAKWIMU ZA RUVU SHOOTING MSIMU HUU UWANJA WA MABATINI
MZUNGUKO WA KWANZA
Ruvu Shooting 3- Prisons (Agosti 24, 2013)
Ruvu Shooting 1-0 Mgambo (Sept 14, 2013)
Ruvu Shooting 1-0 JKT Ruvu (Sept 18, 2013)
Ruvu Shooting 1-0 Rhino (Okt 13, 2013)
Ruvu Shooting 1-1 Kagera (Okt 28, 2013)
Ruvu Shooting 2-2 Mtibwa (Nov 3, 2013)
UWANJA WA TAIFA
Ruvu Shooting 1-1 Simba (Okt 5, 2013)
MECHI ZA UGENINI
Mbeya City 2-1 Ruvu Shooting (Agosti 28, 2013)
Coastal 1-0 Ruvu Shooting (Sept 22, 2013)
Yanga 1-0 Ruvu Shooting (Sept 28, 2013)
Oljoro 2-2 Ruvu Shooting (Okt 9, 2013)
Ashanti 2-2 Ruvu Shooting (Okt 19, 2013)
Azam FC 3-0 Ruvu Shooting (Okt 30, 2013)
MZUNGUKO WA PILI
Ruvu Shooting 1-1 Mbeya City (Jan 29, 2014)
Ruvu Shooting 1-0 Coastal (Febr 15, 2014)
Ruvu Shooting 1-0 Oljoro (Machi 8, 2014)
Ruvu Shooting 2-0 Ashanti (Machi 22, 2014)
UWANJA WA TAIFA
Ruvu Shooting 0-7 Yanga (Febr 22, 2014)
MECHI ZA UGENINI
Mgambo 0-0 Ruvu Shooting (Febr 5, 2014)
Prisons 3-1 Ruvu Shooting (Febr 8, 2014)
JKT Ruvu 0-2 Ruvu Shooting (Febr 12, 2014)
Simba 3-2 Ruvu Shooting (Machi 2, 2014)
Kagera 0-0 Ruvu Shooting (Machi 30, 2014)
Kikosi
cha Thom Olaba cha Ruvu Shooting licha ya kuwa na rekodi mbaya ya
kufungwa magoli 7-0 dhidi ya Yanga msimu huu na kushinda mechi moja tu
ugenini, kimecheza mechi 10 msimu huu kwenye Uwanja wa Mabatini bila
kupoteza hata mechi moja kikishinda nne na sare mbili mzunguko wa kwanza
na kushinda tatu na sare moja mzunguko wa pili.
Masau
Bwire, msemaji wa Ruvu Shooting ameiambia BIN ZUBEIRY kwa simu leo
mchana akiwa Pwani kuwa benchi lao la ufundi limeiandaa vizuri timu
kuhakikisha inalinda heshima ya kutofungwa kwenhye uwanja wa nyumbani na
kuwa timu ya kwanza kuifunga Azam FC msimu huu.
Lakini,
kikosi cha Azam FC kinachonolewa na Mcameroon Joseph Omog kimeonekana
kuwa tishio zaidi msimu huu kikiongoza ligi kwa pointi nne mbele ya
Yanga wanaokamata nafasi ya pili wakiwa na pointi 46, kilikuwa cha
kwanza kuvunja mwiko wa kuifunga Mgambo JKT kwenye Uwanja wa Mkwakwani
mzunguko wa pili huku Simba na Yanga wakichezea vichapo kwenye uwanja
huo.
Azam
FC inahitaji ushindi katika mechi hiyo ya raundi ya 24 ili kujiweka
katika mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa ligi hiyo kwa mara ya
kwanza tangu ipande Ligi Kuu 2007 kwani itakuwa pia na kibarua kigumu
dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mwishoni mwa
wiki.
Mbeya
City haijapoteza hata mechi moja kwenye uwanja huo tangu kuanza kwa
msimu huu Agosti 24 mwaka jana. Azam wataingia uwanjani kesho wakiwa na
kumbukumbu ya kuifunga 3-0 Ruvu Shooting katika mechi yao ya mzunguko wa
kwanza iliyopigwa Uwanja wa Azam Oktoba 30 mwaka jana.
Ruvu
Shooting inakamata nafasi ya sita katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na
pointi 34 ilizozipta katika mechi 23, ikishinda mechi saba, sare tano na
kupoteza saba. Nafasi ya tano inakaliwa na Kagera Sugar wenye pointi 34
pia, tatu nyuma ya Simba katika nafasi ya nne, na 12 nyuma ya Mbeya
City walioko nafasi ya tatu.