IBRAHIMOVIC KUIKOSA MECHI YA MARUDIANO NA CHELSEA DARAJANI BAADA YA KUUMIZWA NA DAVID LUIZ JANA
MSHAMBULIAJI
Zlatan Ibrahimovic ataukosa mchezo wa marudiano wa Robo Fainali ya Ligi
ya Mabingwa Ulaya kutokana na kuumia nyama za paja jana timu yake Paris
Saint-Germain ikiichapa mabao 3-1 Chelsea katika robo fainali ya
kwanza. Mwanasoka
huyo wa kimataifa wa Sweden aliuamia baada ya kugongana na beki wa
Chelsea, David Luiz dakika ya 68 na sasa atatakiwa kuwa nje kwa wiki
tatu. Ibrahimovic
mwenye umri wa miaka 32 ambaye ni tegemeo la PSG katika kampeni za
kutwaa taji la Ulaya na mengine ya nyumbani kukosekana kwake katika
mchezo wa Stamford Bridge Jumanne ijayo litakuwa pigo kwa timu yake. Maumivu makubwa: Zlatan Ibrahimovic akiugulia maumivu jana