MENEJA
WA ENGLAND, Roy Hodgson, amewaita Wachezaji 30 kwa ajili ya Mechi ya
Kirafiki ya Jumatano ijayo dhidi ya Denmark Uwanjani Wembley.
Mechi hii ndio ya mwisho ya England
kabla Hodgson hajateua Kikosi chake kwa ajili ya Fainali za Kombe la
Dunia zitazoanza Juni 12 huko Brazil.
Miongoni mwa Wachezaji walioitwa ni
Fulbeki wa Kushoto wa Southampton, Luke Shaw, mwenye Miaka 18, ambae hii
ni mara yake ya kwanza kuitwa.
Pia wamo Winga wa Liverpool Raheem Sterling, Miaka 19, na Kiungo wa Everton Ross Barkley, Miaka 20.
Vile vile yupo Sentahafu wa Cardiff
City, Steven Caulker, Miaka 22, ambae ni mara yake ya kwanza kuitwa
baada ya Mwaka mmoja na katika Mechi pekee aliyoichezea England ni ile
ya Novemba 2012 ambayo alifunga Bao lakini England ilichapwa na Sweden
kwa Bao 4 za Zlatan Ibrahimovic.
KIKOSI KAMILI:
MAKIPA: Fraser Forster (Celtic), Ben Foster (West Bromwich Albion), Joe Hart (Manchester City), John Ruddy (Norwich City).
MABEKI: Leighton Baines
(Everton), Gary Cahill (Chelsea), Steven Caulker (Cardiff City), Ashley
Cole (Chelsea), Glen Johnson (Liverpool), Luke Shaw (Southampton),
Chris Smalling (Manchester United), Kyle Walker (Tottenham Hotspur).
VIUNGO: Ross Barkley
(Everton), Michael Carrick (Manchester United), Tom Cleverley
(Manchester United), Steven Gerrard (Liverpool), Jordan Henderson
(Liverpool), Adam Lallana (Southampton), Frank Lampard (Chelsea), James
Milner (Manchester City), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Raheem
Sterling (Liverpool), Andros Townsend (Tottenham Hotspur), Jack Wilshere
(Arsenal).
MAFOWADI: Jermain Defoe
(Toronto FC), Rickie Lambert (Southampton), Jay Rodriguez
(Southampton), Wayne Rooney (Manchester United), Daniel Sturridge
(Liverpool), Daniel Welbeck (Manchester United).