
Arsenal watacheza bila Kiungo Jack Wilshere ambae alivunjika Mguu kwenye Mechi ya England na Denmark Juzi Jumatano.
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger,
amegusia kuwa Sentahafu Laurent Koscielny yuko fiti lakini Aaron Ramsey
na Kim Kallstrom bado ni Majeruhi.
Nahodha wa Everton, Phil Jagielka, ana
hatihati kubwa ya kucheza akikabiliwa na tatizo la Musuli za Pajani
[Hamstring] lakini Beki mwenzake, Antolin Alcaraz, yuko tayari kurejea
baada kuwa nje Gemu 6 akikabiliwa na tatizo la Musuli.
Arsenal walifungwa 1-0 na Stoke City
Wikiendi iliyopita kwenye Mechi ya Ligi Kuu England lakini Wenger
anategemea Timu yake kuibuka na ushindi ili waendelee kwenye mbio za
kutwaa Kombe lao la kwanza tangu Mwaka 2005.
Wenger amesema: “FA CUP ni moja ya vitu muhimu kwetu! Tulihuzunishwa kufungwa na Stoke na ni muhimu kushinda Mechi hii!”
Nae Meneja wa Everton Roberto Martinez,
ambae Timu yake ilitoka Sare ya 1-1 na Arsenal kwenye Ligi Mwezi Desemba
Uwanjani Emirates, anaamini Timu yake ipo kwenye wakati mbaya kucheza
na Arsenal wakati huu.
Amesema: “Itakuwa Gemu ya kusisimua! Wao
kucheza Nyumbani ni kitu kikubwa na watajaribu kila kitu kushinda Mechi
hii baada ya kufungwa Mechi iliyopita! Pengine huu ni wakati mbaya
kucheza nao!”