Social Icons

Pages

Monday, 10 February 2014

MWAMBUSI AWATISHIA AMANI SIMBA SC, AWAAMBIA MKIKANYAGA SOKOINE MTAITA MAJI ‘MMA’ KWA MBEYA CITY


BAADA ya timu yake kuinyamazisha Mtibwa Sugar, Kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi amesema nguvu zao sasa wanazielekeza katika mchezo wao ujao dhidi ya Simba utakaopigwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya Jumamosi.
Kikosi cha wageni hao wa ligi kuu juzi kilikizamisha kwa kipigo cha 2-1 kikosi cha kocha Mecky Mexime cha mabingwa wa Tanzania Bara 1999 na 2000, Mtibwa Sugar katika mechi ya raundi ya 17 ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara iliyochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini humo.
, Mwambusi amesema wamejipanga vizuri kwa ajili ya mechi zote tisa zilizobaki wakianzia na Wanamsimbazi Jumamosi.
“Hatujajiandaa kwa ajili ya mechi ya Simba pekee, bali mechi zote zilizopo mbele yetu msimu huu. Mechi yetu inayofuata itakuwa ngumu kwa sababu tutawakosa baadhi ya wachezaji wetu ambao wanatumikia adhabu za kadi, lakini hilo halitupi shida maana nguvu zetu kwa sasa tumezielekeza katika mchezo huo,” amesema Mwambusi.
Mbeya City, ambayo imezinduka baada ya kupunguzwa kasi na Yanga katika mechi yao ya raundi ya 16 ya ligi hiyo, sasa imerudi tena katika nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 34, moja nyuma ya Yanga walioko nafasi ya pili na mbili nyuma ya vinara Azam FC.
Simba imeshuka kwa nafasi moja hadi nafasi ya nne baada ya kukubali kipigo kisichotarajiwa cha bao 1-0 kutoka kwa ‘maafande’ wa Mgambo JKT jijini Tanga jana.
 
FULU VIWANJA