RONALDO YUMO KWA MARA YA 8, SASA MARA 7 MFULULIZO-NI REKODI!
BAADA
kutwaa FIFA Ballon d'Or na kumbwaga Lionel Messi, Cristiano Ronaldo
ameteuliwa kwa mara ya 8 kwenye Timu ya Mwaka ya UEFA na hii ikiwa ni
mara yake ya 7 mfululizo ikiwa ni Rekodi.
BAADA
kutwaa FIFA Ballon d'Or na kumbwaga Lionel Messi, Cristiano Ronaldo
ameteuliwa kwa mara ya 8 kwenye Timu ya Mwaka ya UEFA na hii ikiwa ni
mara yake ya 7 mfululizo ikiwa ni Rekodi.
Lionel hayumo kwenye Kikosi hicho Bora cha Ulaya na pia hamna hata Mchezaji mmoja anaetoka Klabu yake FC Barcelona.
Mabingwa wa Ulaya, Bayern Munich,
wametoa Wachezaji wanne, Real Madrid Wachezaji Watatu, PSG Wawili na
Burissia Dortmu nd na Arsenal ni Mchezaji mmoja mmoja.
Mchezaji pekee anaetoka Ligi Kuu England ni Mesut Ozil ambae sasa anachezea Arsenal akitokea Real Madrid.
Timu hii ya Mwaka ya UEFA imechaguliwa na Watumiaji wa Tovuti ya UEFA ambapo Watu Milioni 6.3 walipiga Kura kuiteua.
KIKOSI KAMILI:
KIPA: Manuel Neuer (Bayern Munich);
MABEKI: Sergio Ramos (Real Madrid), Thiago Silva (Paris Saint-Germain), Philipp Lahm (Bayern Munich), David Alaba (Bayern Munich);
VIUNGO: Franck Ribery (Bayern Munich), Marco Reus (Borussia Dortmund) Mesut Ozil (Arsenal),
MASTRAIKA: Gareth Bale (Real Madrid); Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Zlatan Ibrahimovic (Paris Saint-Germain).