Chelsea wamekamilisha Uhamisho wa Kiungo wa Benfica Nemanja Matic kwa Dau linaloaminika ni kuwa ni zaidi ya Pauni Milioni 20.
Matic, Raia wa Serbia mwenye Miaka 25, amesaini Mkataba wa Miaka mitano na nusu na Chelsea.
Miaka Mitatu iliyopita Matic alitolewa kafara kwa Benfica ili Chelsea imsaini Beki wa Brazil David Luiz kutoka Benfica.
Matic alijiunga na Chelsea akitokea
Klabu ya Slovakia, MFK Kosice, Mwaka 2009 kwa Dau la Pauni Milioni 1.5
na kuichezea Chelsea Mechi mbili tu akitokea Benchi.
Mwezi Agosti 2010, Matic alipelekwa kwa
Mkopo huko Vitesse Arnhem ya Uholanzi kabla kujiunga na Benfica Februari
2011 ili kufanikisha ujio wa David Luiz Klabuni Chelsea.
Akiwa na Chelsea, atavaa Jezi Namba 21