Bosi
wa Tottenham Tim Sherwood amekanusha taarifa kuwa amekuwa katika
mazungumzo ya kumnunua kwa mkopo mlinzi wa Manchester City Joleon
Lescott.
Mlinzi huyo wa kati ambaye amekuwa si pendekezo katika kikosi cha kwanza ndani ya Etihad
Stadium, amekuwa akihusishwa na safari ya kuelekea London ya Kaskazini mpaka mwisho wa msimu.
Hata
hivyo Sherwood amesema hana mpango wa kuongeza nguvu kikosi chake
katika dirisha hili la usajili la mwezi wa Januari, akisisitiza kuwa
atakazania zaidi katika kukiimarisha kikosi chake katika ubora wa
uchezaji na 'fittness'.
‘Sidhani kama tunahitaji mchezaji hapa. Tunahitaji uimara zaidi wa kikosi kwa wachezaji tulionao'.