TIMU
ya soka ya Arsenal imefuzu kutinga Raundi ya Nne ya Kombe la FA baada
ya kuwafunga wapinzani wa London Kaskazini, Tottenham mabao 2-0 Uwanja
wa Emirates.
Santi Cazorla alifuga bao la kwanza dakika ya 31 kabla ya Tomas Rosicky kufunga la pili 62.
Tottenham,
ambayo ilionyesha kuimarika chini ya kocha mpya, Tim Sherwood,
ilizidiwa katika safu ya kiungo na washambuliaji wake Emmanuel Adebayor
na Roberto Soldado wakajikuta hawana madhara uwanjani.
Katika
mechi nyingine, Manchester City ikiwa pungufu ya mchezaji mmoja
ililazimishwa kwenda kwenye mchezo wa marudiano baada ya bao la Scott
Dann kuwapa sare ya 1-1 Blackburn Uwanja wa Ewood Park, kufuatia Alvaro Negredo kutangulia kufunga kipindi ca kwanza
City
ilimpoteza Dedryck Boyata aliyeonyeshwa kadi nyekundu.Katika mechi
nyingine, Barnsley imefungwa 2-1 na Coventry City, Yeovil Town imeifunga
4 - 0 Leyton Orient, Bristol City imetoka 1 - 1 na Watford, Southend
United imeifunga 4 - 1 Millwall, Middlesbrough imefungwa 2-0 na Hull
City, West Bromwich imefungwa 2-0 na Crystal Palace,
Kidderminsterimetoka 0 - 0 na Peterborough.
Doncaster
Rovers imefungwa 3-2 na Stevenage, Stoke City imeifunga 2 - 1 na
Leicester City, Southampton imeifunga 4 - 3 Burnley, Newcastle United
imefungwa 2-1 na Cardiff City, Rochdale imeshinda 2 - 0 dhidi ya Leeds
United, Wigan Athletic imetoka 3 - 3 na Milton Keynes Dons, Norwich City
imetoka 1 - 1 na Fulham.
Aston
Villa imefungwa 2-1 na Sheffield United, Macclesfield Town imetoka 1 - 1
na Sheffield Wednesday, Bolton Wanderers imeshnda 2 - 1 dhidi ya
Blackpool, Everton imeifunga 4 - 0 Queens Park Rangers Brighton
imeifunga 1 - 0 Reading, Grimsby Town imefungwa 3-2 na Huddersfield Town, Ipswich Town imetoka 1 - 1 na Preston North End.

Beki wa Blackburn, Scott Dann akimtungua kipa Costel Pantilimon kuifungia timu yake bao la kusawazisha dhidi ya Manchester City
