
Hull City wamekamilisha kumsaini Straika wa Everton Nikica Jelavic kwa Mkataba wa Miaka Mitatu na Nusu.
Jelavic, Raia wa Croatia mwenye Miaka
28, alitaka kuihama Everton ili apate kucheza mara kwa mara ili aongeze
nafasi yake ya kuchukuliwa na Nchi yake kwenye Fainali za Kombe la Dunia
huko Brazil Mwezi Juni.
Mwaka huu, Jelavic amefunga Bao 3 tu.
Jelavic alijiunga na Everton Miaka
miwili iliyopita akitokea Rangers ya Scotland kwa Dau la Pauni Milioni
5.5 na kuifungia Everton Bao 9 katika Mechi zake 13 za kwanza chini ya
Meneja David Moyes.