
David Moyes amekiri Shitaka la FA
kufuatia kauli yake mara baada ya kufungwa Bao 2-1 na Sunderland katika
Mechi ya Kwanza ya Capital One Cup huko Stadium of Light Wiki moja
iliyopita.
Katika Mechi hiyo, Moyes alikasirishwa na Penati waliyopewa Sunderland na kufunga Bao lao la Pili.
Alidai: “Sasa inabidi tucheze dhidi ya Marefa na Timu pinzani. Ni mbaya sana. Tumeanza kuwacheka. ”
Katika Mechi hiyo, Refa Andre Marriner
hakuashiria Penati hiyo lakini ilibidi aitoe baada ya ushauri kutoka kwa
Mshika Kibendera wake baada Adam Johnson kuanguka wakati akikabiliana
na Tom Cleverley.
Kuhusu Sunderland kupewa Penati Jana,
Moyes alihoji: “Itakuwaje Mshika Kibendera atoe Penati? Refa alikuwa
akiangalia moja kwa moja tukio lile lakini Mshika Kibendera alikuwa
haoni kwani kazibwa na Evra! Mchezaji wetu sisi alipewa Kadi kwa tukio
kama hilo walilopewa Penati! Hata lile Bao la kwanza ile haikuwa Frikiki
ingawa ni kosa letu kutojilinda vizuri kwa Frikiki ile na kuruhusu
Bao!”

Sasa Moyes atakabiliwa na Faini au Onyo baada ya Kesi yake kusikilizwa na Jopo la Fa huku yeye mwenyewe akikataa kuhudhuria.