KOCHA wa viungo wa timu ya taifa ya Ureno, Antonio Gaspar,
amesema anaamini staa wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo atabaki kwenye
ubora wake wa sasa kwa miaka sita ijayo.
Ronaldo amedaiwa kuwa na sifa moja ya kujijali na
kujiweka sawa muda wote na jambo hilo limemfanya Gaspar kuamini supastaa
huyo wa zamani wa Manchester United hatashuka kiwango kwa miaka mingi
ijayo. “Kama atataka, Cristiano atabaki kuwa juu kwa miaka mingi ijayo.
Anaweza kuendelea kucheza kwa kiwango bora hata kwenye umri wa miaka 34 au 35 bila ya wasiwasi,” alisema.
Kocha huyo amemtakia mafanikio staa huyo wa Real
Madrid ambaye kwa sasa ndiye kinara wa mabao katika Ligi Kuu Hispania,
La Liga kutokana kufunga mabao 22.