Social Icons

Pages

Thursday, 30 January 2014

Amir Khan akana kusaliti ndoa

BONDIA Mwingereza, Amir Khan amepuuzia uvumi uliozagaa kwamba amemsaliti mkewe mrembo Faryal Makhdoom, ambaye ni mjamzito kwa kulala na mwanamke mwingine.
Bondia huyo alidaiwa kuwa na uhusiano wa siri wa kimapenzi na mrembo Christie Lee Houle, ambaye aliponda naye raha mwezi uliopita.
Kwa mujibu wa Daily Star, mrembo huyo mwenye umri wa miaka 23 alidai kwamba alilala na bondia huyo nyumbani kwake kwa siku sita kabla ya Faryal kutangaza kwamba wana mtoto wa kike.
Baada ya madai hayo, Khan aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter: “Hahahaa unafanya nicheke.”
Mrembo Faryal naye alitumia ukurasa wake wa Twitter kutetea ndoa yake na kumsifu mumewe huyo
 
FULU VIWANJA