KLABU
ya Arsenal ipo tayari kutoa Pauni Milioni 37 kumnunua kinda mwenye
kipaj Mjerumani ambaye wanaamini atakuwa Robin van Persie mwingine.
Wanajiandaa
kufika bei ya Julian Draxler, mwenye umri wa miaka 20, ambaye
ametambulishwa kama mlengwa mkuu kwa Gunners katika usajili wa dirisha
dogo baada ya kupita huku na kule kusaka vipaji.
Benchi
la Ufundi la Arsene Wenger inaamini Draxler, ambaye anacheza kama
kiungo mshambuliaji katika klabu ya Schalke, anaweza kucheza kama
mshambuliaji pekee wa kati.