KOCHA David Moyes alifanya mazungumzo na
muhusika mkuu wa mijadala ya usajili wa Juventus baada ya kupanga
kuwachukua Paul Pogba na Arturo Vidal.
KOcha huyo wa Manchester United
alikutana bosi wa bodi, Beppe Marotta baada ya mchezo wa Juventus na
Cagliari Jumapili na kujadiliana juu ya uwezekano wa aidha kuwasaini
wote kati ya wachezaji hao anaowataka sana.
Baada ya kusafiri hadi Cagliari na kocha
wa kikosi cha kwanza, Jimmy Lumsden kushuhudia Juve wakitoka nyuma kwa
bao 1-0 na kushinda 4-1 na kuendelea kuongoza msimamo wa ligi ya Italia,
Serie A, Moyes aliweka wazi mipango yake ya kusajili kutoka klabu ya
Turin.
Lakini hadi anarejea Manchester,
alilazimika kukubali kwamba anaweza kumrejesha Pogba pekee Old Trafford
na kuhusu Vidal asubiri hadi mwisho wa msimu.
![]() |
Macho pima: Kocha wa Manchester United, David Moyes alisafiri hadi Italia kuwaangalia vigogo wa Italia Jumapili


Walengwa: Manchester United ipo kwenye mazungumzo na Juve ili kuwasajili viungo Paul Pogba (kushoto) na Arturo Vidal
Zinedine Zidane aliwahi kusema kuondoka
kwa Pogba United miezi 18 iliyopita lilikuwa ni kosa kubwa alilolifanya
kocha wa zamani wa klabu hiyo, Sir Alex Ferguson’s, lakini Moyes
anapambana kumrejesha mkali huyo.
Paris St-Germain pia inamtaka Pogba na
wanaonekana wako tayari kutoa dau linalotakiwa la Pauni Milioni 40
kumnasa. Inafahamika alikuwa tayari kwenda PSG, lakini hajakataa kurejea
Old Trafford.
Kwa sasa, Juventus wako wazi wanasema
hawamuuzi mchezaji huyo. "Kwa upande wetu, hatutakia kumuuza Pogba na
zaidi tumefunga milango juu ya uwezekano wowote wa mtu kutaka kununua
mchezaji kwetu,"