KOCHA
wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amesistiza mchezaji anayetakiwa na
Arsenal, Alvaro Morata hatakwenda popote Januari baada ya kupewa dakika
10 za kucheza kaika ushindi wa 2-0 dhidi ya Osasuna jana kwenye Kombe la
Mfalme.
Mshambuliaji
mwenzake, Jese Rodriguez aliifungia bao la pili Real, na kinda huyo ni
moja sababu za Arsenal kuamini wanaweza kumpata kwa mkopo Morata kutoka
Bernabeu.
"Hatujabadilisha
mtazamo wetu hata kidogo" amesema Ancelotti baada ya ushindi. "Morata
anabaki hapa na hajatuambia sisi kama anataka kuondoka,".

Ushindi:
Kocha wa Real Madrid aliishuhudia timu yake ikiichapa Osasuna 2-0
katika mechi ya kwanza ya 16 Bora Kombe la Mfalme jana
Arsene
Wenger amesema yuko sokoni kutafuta mshambuliaji kufuatia Theo Walcott
kupata maumivu makubwa ya goti na Morata yupo juu katika orodha ya
wachezaji anaowawania.
Olivier
Giroud anatarajiwa kurejea kikosini Arsenal kuelekea mchezo na Aston
Villa Jumatatu, lakini bado Wenger anasema hana washambuliaji wa
kutosha.
Kuimarika
tena kwa Lukas Podolski angalau kutampa ahueni Wenger, wakati Alex
Oxlade-Chamberlain naye akipata ahueni taratibu, lakini kama Arsenal
itapoteza mchezaji mmoja au wawili zaidi, itawagharimu mwishoni mwa
msimu.
