UONGOZI
wa klabu ya Yanga leo umetoa ripoti ya mapato na matumizi kwa kipindi
cha miezi sita tangu Januari 14, 2013 mpaka Julai 14, 2013 ikiwa ni
sehemu ya muendelezo wa kutoa mahesabu hayo kwa wapenzi, washabiki, na
wanachama na jamii kwa ujumla.
Kwa
mujibu wa tovuti ya klabu hiyo, baadhi ya gharama kubwa kwa klabu ni
pamoja na usajili wachezaji na mishahara. Akizungumza na Waandishi wa
habari juu ya mahesabu hayo katibu mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako
amesema mapato makubwa ya klabu yanatokana na viingilio vya mechi na
ufadhili.Juhudi mbalilmbali zinafanyika kuongeza kipato cha klabu kama kuingia mikataba ya ufadhili, kutumia haki miliki za klabu.
Uongozi unajitahid kuweza kudhibiti matumizi ya klabu kama njia moja ya kuhakikisha klabu inajitegemea.
Klabu
bado inaendelea kutegemea ufadhili wa TBL ambao kwa sasa inapata
wastani wa mIL 30.25 kila mwezi, Madhumuni ya ufadhili huu ni kuwezesha
klabu kulipia mishahara ambayo wastani inzaidi mil 60 kwa mwezi. Tayari
klabu imeshaomba mazungumzo na mfadhili kuboresha mkataba huo.
Katika
kipindi cha Januari 2013 hadi Julai 2013 klabu iliweza kupata mil 110
kama zawadi mbalii mbali za ushindi ikiwemo mil 15 kutoka vodacom kwa
kuwa timu yenye nidhamu.
Bado kuna mali za klabu hazija thaminiwa zikiwemo majengo.
