Jose
Mourinho anasisitiza kuwa kinara wa ligi kuu ya soka nchini England
Arsenal hawna maisha kileleni na kwamba anaamini kuwa Manchester
City na Chelsea ndio wapigania taji la ligi hiyo msimu huu.
Mourinho ataanza kazi ya kupunguza pengo la alama nne nyuma ya Arsenal dhidi ya muda mfu ujao.
Mourinho ameeleza kuwa anaogopa zaidi kikosi cha City
‘City
hawana wachezaji wakongwe ukiwaangalia wote pia ni wakomavu na wenye uzoefu mkubwa, Sergio
Aguero, Edin Dzeko, Alvaro Negredo, pamoja na Stevan Jovetic, hawa ni washambuliaji wanne.'
‘Ukielekea
maeneo mengine utaona Yaya Toure, Fernandinho, hakuna aliye na umri
zaidi ya miaka 30 na hakuna mwenye umri chini ya miaka 23. Kikosi
kinaleta raha.

Akizungumzia
washika mitutu Mourinho amesema Manchester United ina alama tisa nyuma
ya Arsenal. Ni pengo kubwa. Tottenham alama 10. ni pengo kubwa lakini
sio pengo kwetu kwa michezo miwili tunaweza kulifuta.