Kocha
wa Sarakasi Bw,Innocent Mathew akiongea na waandishi wa habari (hawapo
pichani), jijini Dar es Salaam kuhusiana na Mchezo wa sarakasi.
Innocent Mathew akiwa kwenye moja ya picha na vijana wenzie.
KOCHA
wa Sakatari,Innocent Mathew ameiomba Serikali kuanzisha Chuo cha
mafunzo ya mchezo huo ili kutoa nafasi kwa vijana wa kitanzania kupata
ujuzi utakaofanikisha kujiajiri wenyewe.
Akizungumza
Dar es Salaam jana na waandishi wa habari, alisema Tanzania ina vijana
wengi wenye vipaji katika michezo mbalimbali ila kinachowakwamisha ni
kutokuwa na sehemu ya kuwaendelea ili kuwa na ufanisi mkubwa
utakaoendana na ushindani kimataifa.
Mathew
ni miongoni mwa vijana 12 wanaounda kundi la Hakuna Matata ambalo
linafanya shughuli za maonesho ya sanaa za jukwaani, ikiwemo uigizaji na
Sarakasi katika visiwa vya Macau pamoja na nchi ya China, alifafanua
kuwa ikiwa Serikali na wadau wa michezo watafanya hivyo itasaidia vijana
wengi kupata fursa ya kujifunza na kuondokana na kuikaa vijiweni.
“Naamini
ikiwa Serikali na wadau wa michezo watatoa hudumu hiyo kwa kuwajengea
vijana vyuo vya aina hiyo itafanya kuwapa fursa ya kujitengenezea ajira
mara baada ya kuhitimu mafunzo yao kwa kuna soko kubwa la mchezo huo nje
ya nchi,” alisema.
Alisema
mfmno unaoweza kutumia ni kwa kutumia kundi lao ambalo lilianzishwa
mwaka 2000 na tangu mwaka 2003 walinza kusafiri katika nchi mbalimbali
kama vile Ujerumani, Australia,Seoul Korea,Ufaransa, Ubelgiji, Uholanzi,
Korea Kusini kwa mkataba wa miaka mitatu na baadae kutua huko Macau,
China.
“Kama
Tanzania inahitaji vijana wake wapate fursa ya kuondokana na umasikini
ni vema ikawatengenezea fursa hiyo ili kufukia mafanikio katika malengo
ya milenia mwaka 2015,” alisema.
Mathew
hivi karibuni alirejea nchini kwa ajili ya mapumziko akitokea China
alikokuwa katika mafunzo mbalimbali ya mchezo huo, amewaomba wadau wa
mchezo huo kujitokeza kumpa sapoti ili kufikia malengo.Chanzo cha habari picha ni full shangwe