Mkurugenzi
wa Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Krismas Bw. Alex Msama
akikabidhi zawadi ya vyakula mbalimbali kwa Halima Mpeta wa kituo cha
Mwandaliwa cha Boko kwa ajili ya sikukuu ya Krismas, Msama amesema kama
ilivyo kawaida ya kampuni hiyo imeamua kutoa kiasi fulani cha mapato
yake ya tamasha hilo na kununua vyakula kwa ajili ya kuwapa zawadi
watoto yatimu ili na wao washerehekee sikukuu ya Krismas vizuri kama
wenzao, vituo vilivyopata zawadi hiyo ya vyakula leo ni Honorata Temeke,
Mwandaliwa Boko, Malaika Kinondoni, Yatima Group Trust Fund ya Chamazi
na Mahabusu ya watoto Upanga vyote vya jijini Dar es salaam,
Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za kampuni hiyo Biafra
Kinondoni jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
wa Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Krismas Bw. Alex Msama
akikabidhi zawadi ya vyakula mbalimbali kwa Mwanaidi Ramadhan wa kituo
cha yatima Malaika cha Konondoni.
Mkurugenzi
wa Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Krismas Bw. Alex Msama
akikabidhi zawadi ya vyakula mbalimbali kwa Alex Mulumba wa kutuo cha
Honorata Temeke
Mkurugenzi
wa Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Krismas Bw. Alex Msama
akikabidhi zawadi ya vyakula mbalimbali kwa Haruna Mtandika wa kituo cha
Yatima Group cha Chamazi wilayani Temeke.
Mkurugenzi
wa Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Krismas Bw. Alex Msama
akikabidhi zawadi ya vyakula mbalimbali kwa Ramadhan Yahya wa Mahabusu
ya watoto Upanga.
Mkurugenzi
wa Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Krismas Bw. Alex Msama
akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi zawadi
ya vyakula mbalimbali.