SUAREZ ASAINI MKATABA MPYA LIVERPOOL

Suarez, ambae Msimu huu amefunga Bao 17
katika Mechi 11 za Ligi Kuu England, alikuwa na Mkataba ambao
ulitarajiwa kumalizika Mwaka 2016 lakini kwenye huu wa sasa atakuwa
akilipwa Pauni 160,000 kwa Wiki hadi mwishoni mwa Msimu na Msimu ujao
kulipwa £200,000 kwa Wiki hadi mwisho wa Mkataba wake.
Kusaini kwa Mkataba huu mpya ni
kubadilika kwa uhusiano kati ya Suarez na uongozi wa Liverpool kwani
Mchezaji huyo alikuwa akishinikiza kuhama mwanzoni mwa Msimu ili ajiunge
Arsenal.
Arsenal ilitoa Ofa mbili kumnunua
ikiwemo ile ya Rekodi ya Pauni Milioni 40,000,001 ili kulazimisha Suarez
ahamie kwao lakini zote hizo ziligomewa na Liverpool.
Baada sakata hilo, Suarez alilazimika kufanya Mazoezi peke yake na baadae kurudishwa kwenye Timu yake ya Kwanza.
Katika muda wake na Liverpool, Suarez
amekumbana na Vifungo viwili virefu pale Desemba 2011 alipofungiwa Mechi
8 kwa kumkashifu Kibaguzi Beki wa Manchester United, Patrice Evra, na
Aprili Mwaka huu kufungiwa Mechi 10 kwa kumng’ata Beki wa Chelsea
Branislav Ivanovic.