TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Desemba 20, 2013
AZAM, SHOOTING TIKETI ZA ELEKTRONIKI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) limeandaa mechi mbili za majaribio ya matumizi ya tiketi za
elektroniki zitakazochezwa Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam.
Mechi ya kwanza itakuwa Desemba 26 mwaka
huu saa 10 jioni ambapo itazikutanisha timu za Azam na Ruvu Shooting.
Mechi nyingine itachezwa Januari Mosi mwakani kwa kuzikutanisha Ashanti
United na JKT Ruvu.
TFF tunatoa mwito kwa washabiki
kujitokeza katika mechi hizo ambapo mbali ya kushuhudia burudani pia
watajionea jinsi mfumo huo wa tiketi za elektroniki unavyofanya kazi.
Kwa kushirikiana na benki ya CRDB ambayo
ndiyo iliyoshinda tenda hiyo ya tiketi za elektroniki, TFF imepanga
vilevile kuandaa mechi nyingine majaribio mikoani kabla ya mfumo huanza
kutumika rasmi Januari 25 mwakani katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu
ya Vodacom (VPL).
PINGAMIZI DIRISHA DOGO MWISHO DES 23
Desemba 23 mwaka huu ndiyo mwisho wa
kipindi cha pingamizi kwa usajili wa dirisha dogo kwa klabu za Ligi Kuu
ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
Katika VPL, Kagera Sugar, Mtibwa Sugar
na Coastal Union ndiyo timu pekee kati ya 14 za ligi hiyo ambazo
hazikuwasilisha maombi ya usajili katika dirisha dogo.
Ashanti United: ndiyo
inayoongoza kwa wachezaji 15 ambao ni Kassim Kilungo, Mohamed Banka,
Bright Obinna, Victor Costa, Juma Mpongo, Juma Jabu, Ally Kondo, Shafii
Rajab, Mohamed Faki, Abubakar Mtiro, Patrick Mhagama, Ally Kabunda,
Hassan Kabuda, Idd Ally na Rahim Abdallah.
Ruvu Shooting: Ally Khan na Jumanne Khamis,
Rhino Rangers; David Siame, John Kauzeni, Salum Mamlo, Jingo Seleman, Darlington Enyinna, Rajab Twaha, Godfrey Mobi na Mussa Digubike.
Mbeya City: Saad Kipanga.
Tanzania Prisons: Dennis Liwanda, Godfrey Pastory, Henry Mwalugala, Jamal Salum na Brayton Mponzi.
Oljoro JKT: Jacob
Masawe, Mansour Ali, Juma Mohamed, Amour Mohamed, Mohamed Ali, Mussa
Nahoda, Benedict Ngasa, Seleman Makame, Shija Mkina, Ali Omar na Shaweji
Yusuf.
Simba: Uhuru Selemani, Ivo Mapunda, Ali Badru, Awadh Juma, Donald Mosoti na Yaw Berko.
Azam: Mouhamed Kone.
Yanga: Hassan Dilunga, Juma Kaseja na Emmanuel Okwi.
Mgambo Shooting; Suleiman Khatib, Bolly Ajali, Amri Sambinga na Issa Ali.
JKT Ruvu: Chacha Marwa, Sino Augustino, Idd Mbaga na Cecil Luambano.
KAMATI YA UTENDAJI TFF DES 23
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itakutana Jumapili (Desemba 23 mwaka huu)
chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jamal Malinzi.
Kikao hicho kitakachofanyika Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam kitapitia ajenda mbalimbali ikiwemo uundwaji wa
vyombo vya haki (Kamati ya Nidhamu, Kamati ya Maadili na Kamati ya
Uchaguzi).
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)