
Fowadi wa USA, Clint Dempsey, anatarajiwa kupimwa afya yake Klabuni Fulham ili arejee tenakuchezea Klabuni hapo kwa Mkopo akitokea Seattle Sounders ya USA.
Dempsey, Miaka 30, aliihama Fulham na
kujiunga na Tottenham kwa Dau la Pauni Milioni 6 Mwaka 2012 na kisha
kuhamia Seattle Sounders Mwezi Agosti Mwaka huu.
Mkopo huu utamsaidia Dempsey kuendelea kucheza hadi Msimu mpya wa MLS, Major League Soccer, utakapoanza tena Machi 8.
Uhamisho huu unatarajiwa kuanza mara tu
Dirisha la Uhamisho litakapofunguka Januari 1 na Bosi wa Fulham, Rene
Meulensteen, ameupokea kwa furaha.
Dempsey alidumu na Fulham kwa Miaka Mitano na Nusu na kuichezea Mechi 184 na kufunga Bao 50