Sergio Aguero nje ya uwanja mwezi mzima
Sergio Aguero atakuwa nje ya uwanja kwa takribani mwezi mzima hizi
zikiwa ni taarifa zilizothibitishwa na bosi wa Manchester City Manuel
Pellegrini.
Mshambuliaji
huyo wa City alipatwa na maswahibu ya maumivu ya msuli katika mchezo wa
ushindi mnono wa mabao 6-3 Jumamosi dhidi ya Arsenal ambao ndio vinara
wa ligi kuu ya England.
Muajentina huyo mwenye mabao 13 ya ligi alifunga bao la uongozi la Gunners kabla ya kutoka mapema kipindi cha pili.
Pellegrini amethibitisha hilo leo mbele ya wanahabari.
City inajipanga kucheza dhidi ya Leicester City katika mchezo wa robo fainali ya League Cup Leo hii