FIFA imetoa Adhabu hiyo ya Kifungo cha
Mechi 10, ambacho kinaanzia Mechi za Croatia za Fainali za Kombe la
Dunia huko Brazil, baada ya Mchezaji huyo kupatikana na hatia ya kutoa
Saluti ya Kibaguzi na Kifashisti mara baada Croatia kuibwaga Iceland
kwenye Mechi ya Mchujo huko Ulaya ambayo iliwapa nafasi kwenda Brazil.
Simunic, mwenye Miaka 35 na ambae ni
Nahodha wa Klabu ya Dinamo Zagreb, alifanya kosa hilo Novemba 19 wakati
Croatia walipoifunga Iceland 2-0 na yeye kunaswa kwenye Video akitumia
Kipaza Sauti kuimba Ubaguzi uliotumika wakati wa Utawala wa Kidhalimu na
Kifashisti wa Masapota wa Nazi wa Ustase.
Katika Taarifa yake FIFA imesema
Mchezaji huyo alitamka Saluti ya Kibaguzi iliyokuwa ikitumika wakati wa
Vita Kuu ya Pili ikiwa ni kuvunja Kanuni ya Nidhamu ya FIFA ya 58 Aya ya
1a.
Adhabu hii kali ya FIFA inaonyesha nia thabiti ya kutokomeza Ubaguzi katika Soka.