Social Icons

Pages

Wednesday, 4 December 2013

MSHAMBULIAJI MPYA WA SIMBA AMALIZA MECHI ZA MAKUNDI BILA HATA GOLI MOJA

MSHAMBULIAJI mpya wa Simba SC, Ali Badru amemaliza mechi za makundi ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge mjini hapa bila ya kufunga bao hata moja.
Kocha Salum Bausi alimuanzisha Badru katika mechi zote mbili za kwanza za Kundi A dhidi ya Sudan Kusini na Ethiopia, lakini baada ya kushindwa kufunga akamuanzishia benchi katika mechi ya jana na Kenya.
Bausi alilazimika kumuingiza Badru dakika ya 51 kuchukua nafasi ya Khamis Mcha ‘Vialli’ wa Azam FC, ambaye naye pia amecheza mechi mbili za makundi bila kufunga.
Hata hivyo, mshambuliaji huyo aliyesajiliwa Simba SC kutoka Canal Suez ya Misri alishindwa kuinusuru Zanzibar na kipigo cha 2-0 kutoka kwa wenyeji Harambee Stars.
Angalau kiungo mpya wa Wekundu hao wa Msimbazi, Awadh Juma Issa aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar, alifunga bao zuri la kufutia machozi dhidi ya Ethiopia, Zanzibar ikilala 3-1.

Kiraka wa Wekundu hao wa Msimbazi, Adeyum Saleh alifunga bao katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Sudan Kusini, wakati bao lingine la Zanzibar siku hiyo lilifungwa na kiungo wa Coastal Union, Suleiman Kassim ‘Selembe’.
 
FULU VIWANJA