Mchezaji afanya mazoezi akiwa na sketi nchini Uskochi ni kituko cha kufunga mwaka. Bofya na usome stori.
![]() |
Partick
Thistle huenda ikawa ni klabu ambayo inapokuwa uwanjani haina la kushangaza
lakini huku nyuma ya pazia inapokuwa katika uwanja wake wa mazoezi vituko ni
sehemu ya kufurahisha ndani ya klabu hiyo ya Uskochi.
Kiungo Gary
Fraser mwenye umri wa miaka 19 akiwa mazoezini alivalia kivazi cha kufungia
mwaka cha rangi ya pinki ambacho kimeunganishwa na sketi iliyokuwa katika rangi
moja.
Fraser kwasasa yuko
kwa mkopo katika klabu ya Bolton Wandarers ya Uskochi.
Inadhaniwa
kuwa Fraser alivalia kivazi hicho akijitofautisha na wenzake kutokana na kwamba
alikuwa mkosefu licha ya kwamba alipokea madharau kutoka kwa wenzake huku
wengine wakidhihaki vazi lake.
Fraser bado
yuko kwa mkopo katika klabu hiyo akitokea katika klabu ya Bolton Wanderers, na
alikumbana na adhabu ya kusimama michezo nane baada ya kushambuliana na mchezaji
mwenzake wa Under-20 katika mchezo dhidi ya Dunfermline.
Fraser
anarejea kutoka kifungoni siku ya mwaka mpya ambapo watakuwa wakielekea kucheza
dhidi ya Celtic, na inadhaniwa kuwa Thistle huenda akaongeza kipindi chake cha
mkopo mpaka mwisho wa msimu.
Kitu kizuri
kwa Fraser ni kwamab angalau katika kivazi chake hicho mguuni alivalia viatu
vyeusi tofauti na hali ilivyo siku hizi hususani katika soka la England ambapo
wachezaji wamekuwa na tabia ya kuvaa viatu vya marangi
mengi.

Begani akilia: Fraser akifarijiwa na mchezaji mwenzake
James Craigen (kushoto) wakati wa mazoezi
Fraser (kulia) alifungiwa
kwa mchezo mbaya wa michuano ya Under-20 dhidi ya
Dunfermline
