MAN UNITED TRANSFER WINDOW: Januari ni kufuma na kumua kikosi, Reus na Herrera katika rada ya Moyes.
Wakati
dirisha dogo la usajili nchini England likiwa linaelekea kufunguliwa na
huku wakuu wa vilabu mbalimbali wakiwa na malengo mbalimbali ya
kufanyia mabadiliko vikosi vyao, kwa upande wa Manchester United mambo
yanaonekana kuwa ni zaidi ya biashara hususani kwa wachezaji wenye
majina makubwa zaidi.
Baada ya kuwakosa wachezaji kadhaa David Moyes kwa hakika atakuwa akitaka kuboresha kikosi chake mwezi ujao wa Januari.
Bosi
huyo mpya atakuwa akisaka wachezaji watakao kuwa na uwezo wa
kusababisha mashambulizi kutokea eneo la kati wakati usajili wa kipindi
cha kiangazi wa kiungo Marouane Fellaini ukionekana kuendelea kutokuzaa
matunda.
What do they need?
United imekuwa ikisaka wachezaji kote duniani ‘world-class
players' karibu katika kila eneo ikiwa ni jitihada za kuweka kikosi katika ubora zaidi.
Kwa muda mrefu United imekuwa ikihitaji damu mpya sehemu ya kiungo, huku wakiendelea kuwa hovyo uwanjani.
Sir
Alex Ferguson alikuwa akijua hili wakati akielekea kustaafu ingawa
hakuwa tayari kulisema, haijulikani ni biashara ya aina gani United
watakwendakufanya mwezi Januari hilo ndilo linalosubiriwa kwa hamu.
David Moyes hatakiwi kufanya makosa mwezi Januari kuimarisha kikosi cha Manchester United chenye soka mbovu kwa hivi sasa.
Andres Iniesta (kulia) hataki kuondoka Barcelona licha ya United kuendelea kuonyeshania.
Marouane Fellaini amekuwa akijitahidi kuonyesha mabadiliko ndani ya kikosi tangu ajiunge kiangazi lakini wapi.
Nani kuingia nani kutoka januari United?
Wakati
wa kiangazi iliyopita United
ilishindwa katika jaribio lake la kumtaka kwa mara nyingine Cristiano
Ronaldo kurejea Old Trafford kabla ya Mreno huyo kuongeza mkataba ndani
ya Real Madrid, na huo ungekuwa ni usajili wa kichwa cha habari kikubwa
ambao wangependa kuufanya.
Garreth
Bale alikuwa ni mmoja wa wachezaji walioshindwa kujiunga na kikosi cha
David Moyes ambaye bado mpaka sasa anataka kwa udi na uvumba saini ya
kiungo Andres Iniesta
na wenzake wawili kutoka Barcelona Cesc Fabregas na Alex Song, pamoja na
Luka Modric wa Real Madrid.
Moyes
pia anaonekana kuvutiwa na mshambuliaji wa Borussia Dortmund Marco Reus
huku swali likiwa bado juu ya mustakabali wa Robie van Persie kusalia
Old Trafford kama ilivyo kwa Wayne Rooney na Javier Hernandez kutokana
na kuibuka kwa mara kwa mara sababu za matishio ya kutaka kuondoka.
Herrera
anaendelea kusalia katika rada ya United tangu alipopoteza kiwango
chake ndani ya Bilbao huku pia United wakiendelea kumfukuzia
mshambuliaji wa Roma aliyethaminishwa kwa pauni milioni £30 pamoja na
Ilkay Gundogan wa Dotmund.
Mawindo
ya meneja wa zamani wa United Sir Alex Ferguson ya kiungo Wesley
Sneijder, ni changuo lingine lakini ugumu unakuja kutokana na umri wa
nyota huyo wa Galatasaray ambaye kwasasa ana umri wa miaka 29.
Nyota wa Borussia Dortmund Marco Reus (kushoto) huenda akajiunga na United Januari.
Viungo Wesley Sneijder (kushoto) na Cesc Fabregas mawindoni United
Nyota
wa Montpellier Remy Cabella huenda akatua United Januari pamoja na
kiungo mwingine wa Everton Ribeiro Cruzeiro, Koke (Atletico Madrid) na
Yohan Cabaye (Newcastle) pamoja na William Carvalho (Sporting Lisbon)
licha ya kwamba orodha imekuwa ikiongezeaka kila wakati.
Mlinzi
wa kushoto Patrice Evra anakaribia kufikia umri wa 33rd na kuna
wasiwasi juu ya Alex Buttner na Fabio kuchukua nafasi yake moja kwa
moja.
Wasaka wachezajin wa United wanahaha kupata huduma ya Alex Sandro wa Porto na mlinzi wa St Etienne Faouzi Ghoulam.
Kuna hali ya wasiwasi katika eneo la ulinzi wa kati ambapo Rio Ferdinand na Nemanja
Vidic wanaelekea ukingoni wa kucheza soka la ushindani wakisaidiwa zaidi na vijana Jonny Evans
na Chris Smalling au Phil Jones katika partnership ya kikosi cha kwanza.
Cristian Zapata wa AC Milan yuko katika orodha ndefu ya wanao waniwa na United.
Ander Herrera windo lingine la United kutoka Athletic Bilbao
Nani wa kuondoka?
Kama United inataka kuziba mapengo
huenda Anderson akawa wa kwanza kuonyeshwa mlango wa kutokea. Ashley
Young pia anaonekana kuisha huku meneja Moyes akionekana kuvutiwa na
Adnan
Januzaj na Wilfried Zaha.
Wanting out? Robin van Persie inaelezwa kuwa si mwenye furaha United
Best ever January buy?
Cantona
aliwasili Novemba ambapo pia mwaka 2006 alisajiliwa Nemanja Vidic na Patrice Evra in the 2006 pamoja na Andy Cole 1995.
January signing to forget?
Wengine ambao wameshasahaulika ni pamoja na Diego Forlan kwa £6.9 mwaka 2002,
Manucho mwaka 2008 na Ritchie De Laet mwka 2009
Wilfried Zaha anatakiwa na vilabu vingi vya Premier League kwamkopo