Social Icons

Pages

Tuesday, 17 December 2013

WILSHERE ASHITAKIWA NA FA!

KIUNGO wa Arsenal Jack Wilshere jana amefunguliwa Mashtaka na FA, Chama cha Soka England, kwa Utovu wa Nidhamu baada kunaswa akitoa ishara ya Kidole kimoja ambayo huchukuliwa kama matusi wakati Arsenal inapigwa Bao 6-3 na Manchester City Jumamosi Uwanjani Etihad.  Tukio hilo ambalo lilitokea katika Dakika ya 67 halikuonwa na Refa Martin Atkinson lakini FA, chini ya taratibu zake mpya za Msimu huu, Jopo la Marefa Watatu wa zamani, ambao ni  Steve Dunn, Eddie Wolstenholme na Alan Wiley, limepitia tukio hilo na kuamua Kosa la Wilshere lingestahili Kadi Nyekundu kama Refa angeliliona.  Kwa vile Jopo lote la Watu watatu limeafikiana, FA imewajibika kumfungulia Mashitaka Wilshere ambae amepewa hadi Jumatano ya leo Desemba 18 Saa 3 Usiku, Saa za Bongo, kujibu Mashitaka hayo.  Hapo Desemba 2011, Luis Suarez alifungiwa Mechi moja baada ya kuwaonyeshea ishara kama hiyo Mashabiki wa Fulham na ikiwa Wilshere atafungiwa hiyo haitakuwa ajabu.  Mchezaji wa kwanza kupitia Jopo la hao Marefa Watatu wa zamani, ambao ni  Tukio la kwanza kupitia mikononi mwa Marefa hao watatu wa zamani ni lile la Mchezaji wa Fulham Sascha Riether alipomkanyaga Adnan Januzaj wa Manchester United bila kuonwa na Refa Lee Probert na Jopo hilo kuamua Riether alistahili Kadi Nyekundu na hivyo akafunguliwa Mashitaka ambayo alikiri na Kufungiwa Mechi 3
 
FULU VIWANJA