Vilabu vya soka nchini Ufaransa vitafanya mgomo mwezi ujao wa Novemba
kwa mara ya kwanza katika miaka 40 kulalamikia mipango ya serikali
kuwatoza kodi ya asilimia 75 wanaopata mapato makubwa
Mgomo huo wa kwanza katika soka la Ufaransa tangu mwaka wa 1972
unatarajiwa kuandaliwa katika wikendi ya mwisho ya Novemba baada ya
vilabu vya nchini humo kupiga kura kwa kauli moja dhidi ya mpango huo
wenye utata wa Rais Msoshalisti wa Ufaransa Francois Hollande wa kutoza
kiwango kikubwa cha kodi.
Rais wa chama cha vilabu vya soka vya Ufaransa – UCPF Jean-Pierre Louvel amesema hakutakuwa na mechi mnamo tarehe 29 Novemba na Desemba 2. Chini ya mapendekezo hayo, makampuni badala ya wachezaji yatahitajika kulipa kiwango cha juu cha kodi kwa niaba ya wafanyakazi waoambao ni wachezaji ambacho kinazidi euro milioni moja.
Louvel anasema vilabu ambavyo vina wasiwasi kuwa uwezo wao wa kuwavutia wachezaji mahiri wanaopata mishahara minono kutoka ng'ambo kucheza nchini Ufaransa utakwama, vitafungua milango yao kwa mashabiki kufafanua kwa wafuasi wao ni kwanini wanahitaji kuchukua hatua hizo kali.