Baada ya kushindataji la ulimwengu la Formula One kwa mara ya nne
mfululizo, changamoto nyingine inayomkabili Sebastian Vettel ni kujaribu
kuwavutia mashabiki wa na kuheshimiwa madereva wenzake
Kijana huyo Mjerumani mwenye umri wa miaka 26, kwa mara nyingine tena
alitawala kuanzia mwanzo hadi mwisho katika mbio za mkondo wa India hapo
jana Jumapili na kuliongeza jina lake katika orodha ya mabingwa wa
Formula One Juan Manuel Fangio na Michael Schumacher kama dereva wa tatu
tu kushinda mataji manne mfululizo yan ulimwengu. Dereva mwingine pekee
kufanya hivyo ni Alain Prost.
Baada ya kumaliza wa kwanza katika mkondo wa jana wa India Grand Prix, ilimbidi atie kidogo mbwembwe katika ushindi wake kwa kufanya mizunguko kadhaa na gari lake huku akitoa wingu kubw ala moshi mweupe kabla ya kuondoka garini mwake, na kuuonesha hesima umati kwa kupiga magoti huku akiinamisha chini kichwa chake. Hata hivyo hatua hiyo ilimsababishia adhabu kwa kutozwa faini pamoja na timu yake ya red Bull ya euro 25,000, kwa kutoelekea moja kwa moja katika sehemu iliyotengwa kumalizia mbio. Hata hivyo adhabu hiyo haijatia doa sherehe za ushindi wake.