skip to main |
skip to sidebar
Bao la Suarez ndilo Goli bora la wiki Ligi ya Mabingwa UEFA, kwa hisani ya Nissan!
Bao hilo lililopatikana kwa jitihada nyingi za mkali
huyo wa Barcelona lilikuwa la sita katika michuano hiyo, wakishinda
dhidi ya Arsenal kutinga robo fainali
Goli la ukweli la Luis Suarez katika mechi ya raundi ya 16 kwa Barcelona mechi ya marudiano dhidi ya Arsenal katika uwanja wa Camp Nou limetajwa kuwa Goli bora la Ligi ya Mabingwa UEFA la wiki na Nissan.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uruguay alifunga goli la umahiri akiwa
ndani ya eneo la hatari la Arsenal kwa kuunganisha pasi nzuri ya Dani
Alves na kumtungua David Ospina kuiwezesha timu yake kushinda 3-1 na
kuiwezesha Barca kutinga hatua ya robo fainali.
Lilikuwa ni goli lake la sita kwa michuano ya Ligi ya Mabingwa UEFA
msimu huu, hivyo kufungana na Lionel Messi, lakini bado yupo nyuma ya
Cristiano Ronaldo ambaye ni kinara wa mabao kwa magoli saba.
Ni mara ya pili msimu huu Suarez ametwaa tuzo hiyo tena, baada ya
kumaliza vizuri kazi dhidi ya Bayer Leverkusen kumpa fursa ya kujitwalia
manyota.
Suarez amewatimulia vumbi waliokuwa wakiwania tuzo hiyo pia; Kingsley
Coman wa Bayern Munich, Diego Costa wa Chelsea, Mohamed Elneny wa
Arsenal na Cuadrado wa Juventus.