Social Icons

Pages

Tuesday, 22 March 2016

BAADA YA KUIRARUA WARRIORS, SAN ANTONIO SPURS YAZIMISHWA KIROHO SAFI.

Kama kuna siku ambazo San Antonio Spurs hawakuamini kilichotokea basi ni alfajiri ya leo katika mchezo dhidi ya Charlotte Hornets. Spurs ambayo ni timu bora ya pili katika NBA kwa rekodi huku ikiwa inaongoza kwa wastani wa ulinzi kwa mchezo ilimaliza robo ya kwanza ikiongoza kwa tofauti ya pointi 23.
Katika sekunde za mwanzo za mchezo kocha wa Hornets, Steve Clifford aliita mapumziko ya kiufundi (timeout) na kuwaasa wachezaji wake kuwa wajaribu kwa nguvu inawezekana.

1171957_1516236975348729_424107121_n
Niliwaambia “Jaribuni kwa nguvu basi, naju wote hapa mnapata pesa nyingi zaidi yangu, najua wote hapa mnaweza mkasababisha nikafkuzwa mkiamua lakini nawaomba mjaribu inawezekana mbona” alisema Clifford huku akicheka baada ya mchezo namna alivyowaeleza wachezaji.
Jeremy Lin alikuja na majibu kwani alifunga pointi 29 huku 15 akizifunga katika robo ya nne na huku akipata mitupo yake yote minne aliiyojaribu ya pointi 3. Hornets ikaichapa San Antonio Spurs kwa jumla ya pointi 91-88, hivyo Spurs wakashindwa kushinda mchezo wao wa 60 wa msimu.
Hii inakuwa mara ya kwanza kwa San Antonio Spurs kupoteza mchezo huku ikiwa inaongoza kwa pointi zaidi ya 23 katika maisha ya Tim Duncan katika klabu hiyo, yaani tangu mwaka 1997.
Jeremy Lin alipata mitupo 11 kati ya 18 aliyojaribu hali iliyosababisha kocha wa San Antonio Spurs mzee mwenye mbwembwe nyingi Gregg Popovich kukiri kuwa hawakuweza kumzuia na kuwa alikuwa katika kiwango cha juu sana.
Hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa timu kumaliza robo ya kwanza ikiwa na pointi 7 au pungufu kisha kumaliza mchezo kwa ushindi tangu Utah Jazz ifanye hivyo kwa New Jersey Nets Dec. 12, 2008.
Courtney Lee alimaliza na pointi 17 , huku  14 akizifunga katika robo ya tatu. Nicolas Batum aliongeza pointi 15, na Cody Zeller alikuwa muhimu sana kwani alidaka rebound 14 kwa upande wa Hornets, ambao walirejea vyema baada ya kupoteza kizembe unaweza kusema dhidi ya Denver Nuggets siku ya Jumamosi.
Kwa Upande wa Spurs Tony Parker alimaliza akiwa na pointi 19, huku LaMarcus Aldridgeakiongeza 18 huku pia akidaka rebound 12. Duncan alimaliza mchezo akiwa na pointi 16 na akidaka rebound 10.
 
FULU VIWANJA