Wachezaji nguli wa zamani duniani wameungana katika harakati za kuondoa umasikini kwa kucheza mechi moja ya hisani mjini Saint-Etienne.
Zidane, Ronaldo de Lima ni moja ya mastaa waliocheza mchezo huo pamoja na Jay Jay okocha Clarence Seedorf, Fabian Barthez pia Gianluca Zambrotta, David Trezeguet na Vladimir Smicer.
Mashabiki wenye bahati katika mji wa Ufaransa wa Saint- Etienne Jumatatu usiku walipata burudani kabambe kutoka kwa mastaa kama Ronaldo wa Brazil na Zinedine Zidane walishiriki katika mwaka wa 12 katika mechi dhidi ya kuondoa Umaskini .
MaLegendary hao wa Mpira wa miguu Ronaldo na Zidane zamani walikua pamoja ikiwa ni pamoja na Clarence Seedorf , Fabian Barthez , Jay- Jay Okocha na Gianluca Zambrotta kwa uchache.
Kama mechi nyingine za kirafiki,Mechi hii ni muhimu sana kwa kutafuta na kuongeza mapato hasa kutokana na viingilio ilikuweza kusaidia watu wanaoishi katika umasikini na hali ngumu ya maisha
Moja ya malengo ya mchezo yalikuja kutoka kwa Seedorf ambaye alipata jina la super cool.Mchezaji wa Zamani wa taifa la Ufaransa, David Trezeguet pia alicheza na alifunga katika mechi, lakini ilikuwa Pierre- EMERICK Aubameyang ambaye aling’aa na kupiga hat-trick wakati upande wake ukipigwa 7-9