![]() |
Mechi hiyo ililazimika kuahirishwa hadi leo baada ya mvua kubwa jana huku wenyeji Stand United wakiwa wanaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na Haruna Chanongo.
Chanongo alifunga bao hilo mbele ya wachezaji na viongozi wa Simba waliokuwa uwanjani hapo wakisubiri kucheza dhidi ya Kagera Sugar, leo.
Katika kipande cha mechi hiyo leo, kila upande ulipoteza nafasi za wazi za kujipatia bao.
Kwa ushindi huo, Stand imefikisha pointi 24 na kuivuka Mtibwa Sugar inayobaki na 23 baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo, moja ikiwa ni dhidi ya Kagera Sugar kwenye uwanja huo wa Kambarage.