
Sterling amegoma kusaini Mkataba mpya na Liverpool huku kukiwa na minong'ono kuwa anataka kwenda Spain kujiunga na Barcelona au Real Madrid huku pia Klabu za England Man City na Arsenal zikitajwa.
Alipoulizwa kuhusu mvutano huo wa Sterling, Mourinho alijibu: "Sipendi Wachezaji ambao hawapendi kucheza na mimi na Klabu yangu. Kila Mchezaji anayo Bei yake. Ukiniuliza kuhusu Eden Hazard kama hataki kuchezea Chelsea basi ipo bei yake!"
Mourinho pia alisema anauelewa msimamo wa Brendan Rodgers aliposema Sterling haendi popote licha ya kuukataa Mkataba mpya.
Sterling bado ana Miaka Miwili kwenye Mkataba wake wa sasa na Liverpool unaomlipa Pauni 35,000 kwa Wiki na aliukataa Mkataba mpya ambao ungemlipa Pauni Lakib1 kwa Wiki na kuibua gumzo kuwa atang'oka Liverpool.