Social Icons

Pages

Sunday, 5 April 2015

malinzi achafuka Shinyanga, Simba wakaidi agizo lake, mechi kupigwa kesho kama kawa!


IMG_20150404_161719
KUMETOKEA sekeseke la nguvu uwanja wa Kambarage Shinyanga kufuatia kupokelewa kwa taarifa kuwa Rais wa Shirikisho la soka Tanzania, TFF, Jamal Malinzi ameagiza kuwa mechi ya Kagera Sugar dhidi ya Simba iliyoahirishwa kesho ichezwe jumatano Aprili 8 badala ya kesho aprili 6 kama ilivyotangazwa jana.

Bodi ya ligi kuu Tanzania bara jana ilifikia maamuzi ya mchezo huo kuchezwa leo kutokana na uwanja kuwa na maji mengi jana, lakini Malinzi, kiongozi wa juu wa TFF akatoa agizo kusogezwa mbele kwa mechi hiyo bila maelezo.

Inaelezwa kuwa baada ya kuahirishwa jana, timu zote zilitumiwa barua pepe kuwa  mechi inachezwa jumatano (leo), lakini ikawa tofauti na ndipo mashabiki wa Simba waliosafiri kutoka Dar es salaam na maeneo mengine wakageuka mbogo.

Wakiwa kwenye Costa zao, waliwasili kwa kishindo uwanja wa CCM Kambarage wakishinikiza kupewa taarifa kwa maandishi iliyotoka kwa Rais Malinzi.
Viongozi wa timu zote walifika ofisi za mpira wa miguu Shinyanga (SHIREFA) na kukubaliana mechi hiyo ichezwe kesho kama ilivyopangwa na kulipuuza agizo la Rais Malinzi.

Bodi imekubaliana na maamuzi hayo kutokana na presha kubwa kutoka kwa mashabiki, hivyo mechi ipo kesho jumatatu jioni.
CHINI YA KAPETI

Taarifa za chini ya kapeti ambazo mtandao huu umezipata ni kwamba kuna mjumbe mmoja wa kamati ya utendaji ya Simba (jina tunalihifadhi) ameandaa Mabonanza ya Simba huko Roliya Mara.

Mjumbe huyo ana mpango wa kugombea ubunge, hivyo Mabonanza hayo yana maana kubwa kwake kisiasa. Lengo la kuipeleka Simba ni kuendelea kuwashawishi wananchi wa huko.

Baada ya kuahirishwa kwa mechi jana ratiba ya Mabonanza hayo yaliyotarajiwa kuanza leo jumapili imevurugika na ndipo kiongozi huyo akampigia simu rafiki yake Malinzi akiomba aamuru mechi ichezwe jumatano ili Simba iende huko kwanza halafu irudi Shinyanga kucheza mechi jumatano.
Malinzi akafanya hivyo, lakini mambo yamekuwa magumu kweli kweli baada ya Watu kuchachamaa.

Ratiba ya Simba ilikuwa hivi: Baada ya mechi jumamosi walitakiwa kuondoka kwenda Mwanza na kunywa Chai asubuhi na hatimaye kwenda Roliya Mkoani Mara jumatatu asubuhi kucheza Bonanza na kuzindua Tawi.

Jumanne walitakiwa kurudi Musoma na kuzuru kaburi la Baba wa Taifa Butiama, baaada ya hapo walitakiwa kurudi Musoma mjini kucheza mechi na Musoma Kombaini.

Jumatano walitakiwa kusafiri kurudi Dar.

chanzo .shafidauda
 
FULU VIWANJA