Ile vuta nikuvute ya La Liga huko Spain kati ya Miamba FC Barcelona na Real Madrid kugombea Ubingwa na zile mbio za Nyota wa Klabu hizo, Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, kuwania Pichichi, Tuzo ya Mfungaji Bora, Leo tena zinaendelea.
FC Barcelona, ambao wapo kileleni mwa La Liga, watakuwa kwao Nou Camp kucheza na UD Almeria wakiongozwa na Supastaa wao Lionel Messi mwenye Bao 32 kwenye La Liga Msimu huu akisaka kufuta ukame uliomkuta Mechi iliyopita ambapo Timu yake iliifunga Celta Vigo Bao 1-0 kwa Bao la Jeremy Mathieu.
Real Madrid, ambao wako Nafasi ya Pili nyuma ya Barca, watakuwa Ugenini Estadio Teresa Rivero lakini Jijini Madrid kucheza na Rayo Vallecano wakiongozwa na Mchezaji Bora Duniani Cristiano Ronaldo ambae baada kufifia aliibuka Wikiendi iliyopita na kupiga Bao 5 wakati Real inaibonda Granada 9-1 na Mabao yake hayo kumfanya ampiku Messi na yeye kutwaa uongozi wa La Liga sasa akiwa na Bao 36.
LA LIGA
Msimamo-Timu za Juu:
1. Barcelona Mechi 29 Pointi 71
2. Real Madrid Mechi 29 Pointi 67
3. Atletico Madrid Mechi 30 Pointi 65
4. Valencia Mechi 29 Pointi 61
5. Sevilla Mechi 30 Pointi 61