Social Icons

Pages

Wednesday, 8 April 2015

COPPA ITALIA: JUVE WAINYUKA FIORENTINA 3-0, HAO FAINALI....!!



COPPA-ITALIAWakicheza Ugenini bila ya Nyota wao bora, Andrea Pirlo, Paul Pogba na Carlos Tevez, Juventus, chini ya Kocha Massimiliano Allegri, Usiku huu wameipindua kipigo cha Nechi ya kwanza na kuichapa Fiorentina 3-0 na kutinga Fainali ya Coppa Italiana.
Hii ni nafasi murua kwa Juve kutwaa Dabo Msimu huu kwani kwenye Ligi Serie A wao ndio Vinara wakiwa Pointi 14 mbele.
Bao za Juve, ambao walifungwa 2-1 katika Mechi ya kwanza zilifungwa na Alessandro Matri, Roberto Pereyra na Leonardo Bonucci.
VIKOSI:
Fiorentina (Mfumo 3-5-2): Neto; Stefan Savic; Gonzalo Rodríguez, José María Basanta; Joaquín, Mati Fernandez, Alberto Aquilani, Borja Valero, Marcos Alonso; Mario Gomez, Mo Salah.
Juventus (Mfumo 4-3-1-2): Marco Storari; Simone Padoin, Leonardo Bonucci, Giorgio Chiellini, Patrice Evra; Arturo Vidal, Claudio Marchisio, Stefano Sturaro; Roberto Pereyra; Alessandro Matri, Álvaro Morata.
Coppa Italia 
 
FULU VIWANJA