Mkuu
wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Yanga, Jerry Muro, amekanusha uvumi wa
viongozi wa timu hiyo kumtimua kambini mshambuliaji wao, Danny Mrwanda na kudai
kulikuwa na sababu kadhaa za mchezaji huo kuondoka kambini lakini siyo kwamba
alifukuzwa.
Muro
amesema sababu ya kwanza ya Mrwanda kuondoka kambini kwenye Hoteli ya Tansoma
iliyopo Kariakoo jijini Dar ni kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa malaria.
“Mrwanda
hakufukuzwa, ni mgonjwa lakini pia ameondoka kambini kwa kuwa anatumikia adhabu
ya kadi nyekundu aliyoipata katika mechi dhidi ya BDF,” alisema Muro na
kuongeza:
chanzo salehe jembe