Huko Gaborone, Botswana hapo
Jana , Yanga ilifungwa Bao 2 - 1
na BDF XI kwenye Mechi ya
Pili ya Raundi ya Awali ya
Mashindano ya CAF ya Kombe
la Shirikisho lakini wamesonga
na kutinga Raundi ya Kwanza
kwa Jumla ya Mabao 3- 2
baada ya kushinda Mechi ya
Kwanza 2- 0 Mjini Dar es
Salaa.
Kwenye Mechi ya Jana, Yanga
walitangulia Bao 1 - 0 hadi
Mapumziko alilofunga Mrisho
Ngassa lakini BDF XI Kipindi
cha Pili walifunga Bao 2 na
Gemu kwisha 2- 1 huku Yanga
pa wakiwa Mtu 10 baada ya
Danny Mrwanda kupewa Kadi
Nyekundu katika Dakika ya 70.
BDF XI pia walicheza Mtu 10
kuanzia Dakika ya 21 baada ya
Mchezaji wao Mparithe
kutolewa kwa Kadi Nyekundu .
Katika Raundi ijayo, Yanga
watacheza na Mshindi kati ya
Platinum ya Zimbabwe na
Sofapaka ya Kenya ambao
wanarudiana Wikiendi hii huku
Platinum wakiwa washindi wa
Bao 2 - 1 katika Mechi ya
Kwanza iliyochezwa Nairobi .
Leo ,i Timu nyingine mbili za
Tanzania , Azam FC na KMKM ,
zitakuwa Viwanjani kwenye
Mechi zao za Pili za Raundi ya
Awali ya CAF CHAMPIONS LIGI
wakati Polisi ya Zanzibar
itacheza Mechi yake ya Pili ya
Raundi ya Awali ya
Mashindano ya CAF ya Kombe
la Shirikisho hapo Jumapili .