MABINGWA
wa Italy, Juventus, wakicheza bila ya Nyota wao Carlos Tevez, Andrea
Pirlo na Gigi Buffon, waliopumzishwa wakati Arturo Vidal akiwa mgonjwa,
waliifumua Verona Bao 6-1 kwenye Mechi ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya
Coppa Italiana. 

Hadi Mapumziko Juve walikuwa mbele Bao 3-0 kwa Bao mbili za Sebastian Giovinco na moja la Roberto Pereyra.
Kipindi cha Pili, Paul Pogba akapiga Bao la 4 na kuifanya Juve iongoze 4-0 lakini Nene akafunga Bao kwa Verona na Gemu kuwa 4-1
Alvaro
Morata akaipa Bao la 5 Juve kwenye Dakika ya 63 kwa Penati baada ya
Rafael Marquez kumwangusha Sebastian Giovinco na la 6 kufungwa na Coman.
Juve sasa wametinga Robo Fainali na watacheza Nyumbani na Parma ambayo iliifunga Cagliari 2-1.
Mechi za Robo Fainali zitachezwa Februari 4.