Social Icons

Pages

Sunday, 24 August 2014

LOGA: SINA KAZI, NASUBIRI TIMU



Kocha Zdravko Logarusic amesema bado hajafanikiwa kupata ajira mpya.

Loga raia wa Croatia, baada ya kufutwa kazi na Simba, sasa anaendelea na mapumziko huku akisubiri ajira mpya.
“Nitaendelea kutafuta na pia kusubiri kama kuna timu zitakuwa zinanihitaji.
“Lakini sasa bado kidogo, hakuna timu wala sina ajira mpya,” alisema Loga akifafanua taarifa za kwamba Gor Mahia ya Kenya imeanza mazungumzo naye.
Loga aliifundisha Simba kwa nusu msimu, lakini baada ya kuingia mkataba mpya wa mwaka mmoja, hakupata nafasi ya kuendelea kuitumikia.
 
FULU VIWANJA