Kocha msaidizi wa timu ya wachezaji wa zamani wa Tanzania Eleven, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’,
juzi alitoa kituko kwa kumchapa
kofi mwandishi ambaye (siyo wa Championi) alikuwa akimrekodi bila idhini yake
baada ya kumaliza mazoezi yanayofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar.
Julio
alifanya kitendo hicho baada ya kugundua anarekodiwa pasipo mwenyewe kujua,
jambo ambalo lilimkera, hivyo kuchukua uamuzi huo kama alivyofanya staa wa
Argentina, Diego Maradona hivi karibuni.
Julio alizungukwa na kundi kubwa la mashabiki ambapo alikuwa akipiga nao soga mbalimbali.
Wakati mazungumzo yamekolea, kocha huyo alimpokonya simu kijana aliyekuwa
karibu yake na kuitupa mbali na kisha kumpiga kibao na kumsindikizia na maneno
yake yalee ya mbwembwe.
“Haiwezekani
we ufike unirekodi tu mimi wakati nipo kwenye mazungumzo binafsi,” alisema
Julio na kuungwa
mkono na wale aliokuwa akizungumza nao.